Safari ya maisha ndefu. Maendeleo ya kielimu yanahitaji uvumilivu, kujituma na kuwajibika ili kufikia kilele cha mafanikio ambacho mtu hukitarajia. Leo hii ninapoandika ni mwaka sasa kwa baadhi ya wanachuo, wengine ni mwaka wa pili, lakini njia ni moja tu, "kuelekea mafanikio ya kitaaluma na ufundishaji wenye tija kwa wote wanaosoma ualimu". Ndiyo maana nawaandikieni, kwanza kuwapongezeni kwa kumaliza mwaka kwa mafanikio, pili kuwaombeni sasa kwenda kuwajibika ipasavyo kuhakikisha wanafunzi mtakaowafundisha, mnawapa maarifa ya kutosha kwa kadri ya mahitaji yao.
Jambo la msingi hapa ninalohitaji tulizungumzie, Ni kwa kiwango gani mwalimu anawajibika kwa mwanafunzi wake. Ni heshima ipi anayopaswa kuitoa kwake, miongozi ipi na anapaswa kumtimizia matakwa yapi? tukiweza kuyatafakari haya yote.....njia yetu itakuwa yenye mafanikio. Mungu awabariki na nendeni mtangaze YOWE la Babu.