KIGODA cha marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kilichozinduliwa mwaka jana kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na kukaliwa na Profesa Issa Shivji, mwaka huu kitashuhudia ugeni mkubwa wa kusherehekea kumbukubu ya kuzaliwa kwa kiongozi huyo maarufu duniani.
Sherehe hizi zitaanza Aprili 13
Sherehe hizi zitaanza Aprili 13
hadi 17 na kutengeneza kitu kijulikanacho kama wiki ya tamasha la Mwalimu; zitapambwa na mihadhara ya kisomi, majadiliano na kuelimishana juu ya mawazo ya mwalimu, matendo yake na hasa juu ya mapenzi yake juu ya Umoja wa Afrika.
Kaulimbiu ya tamasha hili itakuwa: Binadamu wote ni sawa, Afrika ni moja na Afrika ni lazima iungane.
Katika tamasha hili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kitazindua Mhadhara wa Mwalimu wa kila mwaka. Na mwaka huu Mhadhara huu, utatolewa na mwandishi maarufu na mwenye nishani ya uandishi Wole Soyinka, ambaye atachambua na kuchochea majadiliano juu ya ubeberu mamboleo.
Tumemsoma sana Wole Soyinka enzi za kale na leo hii watoto na wajukuu bado wanasoma mawazo ya Wole Soyinka. Itakuwa ni heshima ya pekee kumsikiliza akizungumza juu ya Mwalimu, kuuchambua ubeberu mamboleo na kukitukuza Kiswahili, lugha anayoamini inaweza kuliunganisha Bara la Afrika.
Mbali na Wole Soyinka, kwenye tamasha hili kutakuwepo pia wageni wengine kama mtoto wa marehemu Nkrumah, Gamal Nkrumah na mtoto wa Franzt Fanon, Olivier Fanon. Wageni wengine watatoka Ghana, Kenya, Uganda na Afrika ya Kusini.
Naandika makala hii kuwashawishi na kuwaomba Watanzania kufika kwa wingi kwenye tamasha hili. Litakuwa ni jambo la kushangaza sana wageni kuwa wengi kwenye tamasha hili zaidi ya wenyeji.
Kuna usemi kwamba nabii, hasifiki nyumbani kwake; msemo huu uwe tofauti kwetu sisi, maana kusema kweli tuna mengi ya kujivunia kwa Mwalimu wetu, na hasa juu ya Tanzania yetu huru.
Ni vigumu kuiongelea Tanzania huru, bila kumtaja marahemu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Ni ukweli kwamba watu wengi walishiriki kuleta uhuru wa Tanzania, lakini aliyekuwa na mtazamo na kuona mbali ni Mwalimu. Historia inatufundisha na hadi leo hii tunajionea wenyewe.
Kuhusu uhuru wa Tanzania na Watanzania, Mwalimu Nyerere hakuyumba wala kugeuka nyuma. Tunaukumbuka msemo wake wa “Nikigeuka nyuma, nitageuka jiwe…” Huu ni msimamo wa mtu makini, aliyejikomboa kifikra, mzalendo na mwenye kuangalia mbali. Kuna mifano mingi inayoonyesha jinsi Mwalimu alivyokuwa na vision na kuangalia mbali. Mfano, usiku wa kuamkia Desemba 9 1961, Mwalimu alitamka hivi:
“ Mtalala malofa na mtaamka malofa. Mtalala kama watawaliwa lakini mtaamka kama watu huru na mnaojitawala. Msikubali mtu yeyote awanyang’anye uhuru wenu.”
Kama alivyosema Mwalimu, uhuru ulipatikana, na yeye alitumia nguvu zake zote kuulinda uhuru wetu. Na si kuulinda uhuru wetu tu, alihakikisha nchi nyingine za Afrika zinapata uhuru kama wa kwetu.
Si lengo la makala hii kuelezea mchango wa Mwalimu katika ukombozi wa Afrika, ila ni kudokeze tu jinsi Mwalimu alivyouthamini uhuru. Si uhuru wake na watu wake, bali hata uhuru wa jirani zake. Tunakumbuka alivyotufundisha kwamba kama jirani yako si uhuru, uhuru wako na wewe pia uko mashakani.
Haya tuliyaona kutokana na mapambano ya ukombozi kusini mwa Afrika, sasa imebaki kuwa historia.
Uhuru ulipatikana, lakini ulofa, ulibaki palepale. Watu wengi hawakuwa na elimu, ajira, umaskini ulikuwa ni wa kutisha na maradhi yaliwashambulia watu kwa kasi. Kwa kupambana na ulofa, kitu ambacho pia alikifanya kwa nguvu zake zote, Mwalimu, aliwatangaza maadui wa Mtanzania: ujinga, maradhi na umaskini.
Vitu hivi aliviona kama kizingiti kikubwa kwa Mtanzania kufikia maendeleo. Ili kupambana na maaduia hawa watatu, na kuutokomeza ulofa, na kuyakaribisha maendeleo, Mwalimu alizitangaza silaha za kutumia: Ardhi, siasa safi, watu na uongozi bora.
Maisha yote ya Mwalimu Nyerere, alipambana na ulofa na kuulinda uhuru wa Tanzania. Aliyafanya haya kwa uaminifu mwingi. Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ilizaliwa kutokana na lengo lake hili la kupambana na ulofa na kuulinda uhuru wa Tanzania.
Makosa ya hapa na pale yalijitokeza wakati wa kutekeleza siasa ya ujamaa na kujitegemea, mfano kuwahamishia watu kwenye vijiji vya ujamaa bila mipango inayoeleweka vizuri, kuharibu mfumo wa jumuia za kiraia zilizosukuma aina fulani ya maendeleo wakati wa ukoloni na kuusambaratisha mfumo wa serikali za mitaa.
Mfano, vyama vya ushirika vilikuwa na nguvu kubwa (vyama vya wakulima wa pamba, kahawa nk) baadhi ya vyama hivi vilijulikana dunia nzima kwa kuwa na utawala bora na nguvu za kifedha.
Ingawa sasa hivi makosa haya yanalighalimu taifa letu, lakini yalifanyika kwa nia njema, haya yanaitwa makosa yenye heri.
Kwa namna ya pekee siasa ya ujamaa ilipambana na ulofa na kuulinda uhuru wa Tanzania. Hili ndilo jambo la msingi, kwamba mtu anajikomboa kifikra na kuwa macho kulinda uhuru wake.
Ni bahati mbaya kwamba wale waliokuwa wamemzuguka Mwalimu na watekelezaji wake hawakuyaelewa vizuri malengo yake. Ndiyo maana badala ya kuuboresha mfumo wa siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, wameamua kuuzika. Sasa hivi analaumiwa Mwalimu Nyerere, kwa siasa ya ujamaa, wakati waliokuwa wakiisimamia siasa hiyo kwa unafiki wanaendelea kutanua na kuila nchi!
Awamu ya kwanza ya uongozi wa taifa letu ilisaidia sana kuimarisha misingi ya taifa letu, maadili ya taifa letu, umoja wa taifa, mshikamano wa taifa, lakini pia kujaribu kuwafanya Watanzania wajione kwamba ni taifa huru. Pamoja na dosari zilizojitokeza wakati wa Awamu ya Kwanza, hakuna anayeweza kupinga mafanikio niliyoyataja hapo juu.
Awamu ya pili ya mzee Ali Hassan Mwinyi, ilifungua milango ya biashara.
Kama hii ilisaidia kupambana na ulofa, kujenga moyo wa kutetea uhuru wetu na uzalendo, historia itaeleza.
Jambo kubwa alilolifanya mzee Mwinyi ni kuimarisha demokrasia katika nchi yetu. Chini ya uongozi wake, Tanzania iliingia katika mfumo wa vyama vingi, pamoja na kwamba mpaka hivi sasa hatujafikia kiwango ambacho kila mmoja anatosheka, lakini ukweli ni kwamba misingi madhubuti imeanza kuwekwa na imewekwa chini ya Awamu ya Pili.
Awamu ya Tatu ilishughulikia zaidi mambo ya uchumi na imefanya kazi nzuri. Jambo linaloshangaza sana ni kwamba zaidi ya miaka arobaini baada ya uhuru wetu, ulofa unaongezeka na umaskini unashika kasi ya kutisha.
Na uhuru wetu unaanza kutia shaka kiasi cha mtu kuhoji kama kweli ni uhuru ule aliousema Mwalimu Nyerere, uhuru wa kuacha kutawaliwa na watu wakaamua mambo yao wenyewe, au ni uhuru wa bendera.
Awamu ya Nne ina falsafa ya Kasi mpya, Nguvu mpya na Ari mpya. Hadi sasa tunashuhudia kazi yake na hasa kuwashughulikia mafisadi na jitihada za kujenga uchumi ili kuboresha maisha ya kila Mtanzania.
Swali ambalo linajitokeza kwenye awamu zote za uongozi wa taifa letu, ukitoa ile awamu ya Mwalimu ni: Je, Tanzania bado ni huru? Ulofa umetokomea? Je, Watanzania bado tunazingatia fikra za Mwalimu kwamba: Binadamu wote ni sawa, Afrika ni moja na Afrika ni lazima iungane?
Maswali haya na mengine mengi ni kati ya hoja za kujadiliwa katika tamasha la Mwalimu. Tufike kwa wingi kwenye tamasha hili chini ya Kigoda cha Mwalimu, ili tujadiliane na kuelimishana.

No comments:
Post a Comment