The Prevention and Combating of Corruption BUreau
- Maelfu watembelea banda hilo na kuelimishwa
Juni 16-23, 2011 TAKUKURU ilishiriki Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam na kutembelewa na wananchi 2,917, kati yao wanaume walikuwa 2,120 na wanawake 797. Maadhimisho ya haya yalikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na yalibeba kauli mbiu “Mkataba wa Kanuni na misingi ya Utumishi wa Umma Barani Afrika ni Chachu ya kuimarisha Utoaji Huduma bora kwa Umma”. TAKUKURU ilielimisha kupitia ujumbe dhidi ya rushwa uliosema “Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, Ziingatia Maadili ili Kuimarisha Huduma Bora”.
Katika maonyesho hayo TAKUKURU ilielimisha jamii juu ya dhana ya rushwa, madhara yake na namna ya kuidhibiti kwa kutoa maelezo kuhusu majukumu na utendaji kazi wa wake, kujibu maswali ya wananchi, kugawa machapisho, kupokea changamoto na maoni ya wananchi, kujenga mahusiano mema na wadau kwa kuwaelimisha jinsi tunavyoweza kushirikiana katika kutekeleza jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa nchini. Taasisi ilitumia fursa hiyo pia kupokea taarifa za vitendo vya rushwa, ambapo kero mbalimbali za rushwa zinazowakabili wananchi zilitolewa na kupokelewa na Taasisi inaendelea kuzifanyia kazi.
Aidha wananchi walipata fursa ya kutoa maoni ambapo waliashauri kuwa adhabu za makosa ya rushwa ziongezwe kwa kuwa rushwa inasababisha hasara kubwa kwa Serikali. Pia wananchi waliitaka TAKUKURU iongeze bidii ya kutoa elimu kwa kuwatembelea wananchi na kusikiliza kero zinazowasumbua. Vilevile, wananchi waliitaka Taasisi kuelekeze nguvu ndani ya Vyama vya Siasa watika wa chaguzi.
Ushiriki wa TAKUKURU katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma umetoa fursa ya kutathmini utendaji wake wa kazi na pia kushirikisha wananchi katika kuzuia na kupambana na rushwa kwa njia ya wao kutoa taarifa za rushwa na maoni kuhusu jinsi ya kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa nchini. Ni wazi kuwa kuendelea kushiriki katika maaadhimisho kama haya kunaisogeza TAKUKURU karibu zaidi na wananchi.
Ni matarajio ya TAKUKURU kuwa wananchi wameelimika hivyo hawatajihusisha na vitendo vya rushwa na watendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa.
Maadhimisho ya mwaka huu yalihudhuriwa na nchi 7 ambazo ni Kenya, Zambia, Zimbabwe, Afrika ya Kusini, Korea ya Kusini, Oman na Tanzania. Jumla ya wananchi 2,917 walitembelea banda la TAKUKURU ambapo wanaume walikuwa 2,120 na wanawake 797. Machapisho 7,159 yenye ujumbe dhidi ya rushwa yaligawiwa kwa wananchi yakiwemo majarida, vipeperushi, ripoti za tafiti na nakala za Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007.
wow it is nice work done by our members
ReplyDelete